Yanga, Namungo wagawana alama dimba la Majaliwa

Namungo FC leo Jumapili imefanikiwa kuvuna alama moja dhidi ya Mabingwa wa kihistoria wa TPL Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara uliopigwa dimba la Majaliwa Lindi kufuatia sare ya goli 1-1.

Yanga ilianza kuongoza kunako dakika ya sita ya mchezo goli likifungwa na Tariq Seif Kilakala akimalizia majalo ya Juma Abdul, goli lililodumu mpaka tamati ya dakika 45 za kwanza.
Kipindi cha pili Namungo FC walipata bao la kusawazisha kupitia kwa Bigirimana Blaise dakika ya 62. Sare hiyo inaifanya Namungo kufikisha pointi 50 ikiwa nafasi ya nne huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu na pointi 51.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends