Yanga ndani ya 16 za mwisho za ASFC baada ya kuwashinda Prisons

Yanga imefuzu hatua ya 16 bora ya Kombe la ASFC baada ya kuifunga timu ya Jeshi la Magereza Tanzania Prisons kutoka Mbeya goli 2-0 katika mchezo uliopigwa dimba la Taifa leo Jumapili.

Mechi hiyo iliyokuwa ya Kombe la Shirikisho, imeshuhudiwa mabao ya Yanga yakiwekwa kimiani na Bernard Morrison aliyefunga kwa njia ya penati kunako dakika ya 10 ya mchezo pamoja na Yikpe Gnemien aliyefunga kipindi cha pili akimalizia pasi safi ya Morrison aliyekuwa nyota wa mchezo huo.

Ushindi huo umewafanya Yanga kusonga mbele ambapo hivi sasa watakutana na Gwambina FC katika mechi ijayo ya hatua ya 16 bora au mtoano.

Safari ya Yanga ilianza kwa kuifunga Iringa United goli 4 wakati Wajelajela Tanzania Prisons wakiitoa Mlale.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends