Yanga SC kujipima nguvu kwa African Lyon

Yanga SC leo Jumapili, Novemba 15 kitakuwa na kibarua cha kumenyana na African Lyon kwenye mchezo wa kirafiki uliopangwa kuchezwa katika dimba la Azam Complex jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa moja usiku.

Yanga ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Tanzania VPL imeamua kupata mchezo huo kwa ajili ya kutesti mitambo ya timu hiyo kuelekea kwenye mechi zijazo za ligi.

Timu hiyo ya Wananchi inayonolewa na kocha Cedric Kaze raia wa Burundi, mwenye tuzo ya kocha bora Oktoba kitashuka uwanjani kikiwa na kumbukumbu za kuvuna alama moja katika mchezo uliopita wa Ligi dhidi ya Simba Novemba 7 baada ya sare ya 1-1.

Viingilio vya mchezo huo ni 3,000 kwa mzunguko na VIP ni 5,000.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends