Yanga Yaanza Kuuweka Ubingwa Rehani, Yabanwa na Prisons

347

Vinara wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Yanga SC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu, mtanange uliopigwa dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Ukiwa ni mchezo wa tatu bila kufunga bao, Yanga waliweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga magoli ikiwemo kupata penati ambayo ilikoswa na kinara wa ufungaji ndani ya klabu hiyo Mkongo, Fiston Kalala Mayele.

Kwa sare hiyo ya tatu mfululizo, Yanga inafikisha pointi 57 katika mchezo wa 23 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi 11 zaidi ya mabingwa watetezi, Simba ambao wenyewe wana mechi moja mkononi.

Tanzania Prisons inafikisha pointi 23, mechi ya 23 nafasi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.

Author: Asifiwe Mbembela