Yanga yaendeleza ubabe Morogoro mechi ya kirafiki

Yanga imeendelea kushinda mfululizo mechi zake za kirafiki za kujiandaa na msimu ujao wa mashindano ambapo leo Julai 23 imeweza kuitwanga Moro Athletic Academy ya Morogoro kwa mabao 7 – 0. Yanga ambayo imejikita na maandalizi yao ndani ya Jiji kasoro Bahari Morogoro imekuwa ikifanya vizuri kwenye michezo hiyo ikiwa chini ya Kocha msaidizi Noel Mwandila ikijiandaa na msimu mpya wa 2019/20.

Klabu hiyo yenye Makao yake maeneo ya Jangwani Kariakoo, ilitawala kwa kiasi kikubwa mchezo huo huku wakitandaza soka walivyotaka. Kalamu ya magoli katika mchezo huo ilianzishwa na Mnyarwanda Sibomana alifanikiwa kufunga mabao matatu kwa maana ya hat trick, Sadney Ukhirob kutoka Guinea amefunga goli 2, na mlinzi Lamine Moro goli 1 na Juma Balinya kutoka  goli 1.

Huo unakuwa mchezo wa tatu mfululizo kwa Yanga kuibuka na ushindi mnono huko Morogoro ambapo hivi karibuni imeshinda dhidi ya Moro Kids

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends