Yanga yagawana alama na Dodoma Jiji

Yanga imegawa alama moja nayo akichukua moja na kuiacha moja dimba la Jamhuri Dodoma kutokana na sare tasa katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Leo Jumapili Julai 18.

 

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi imepata pointi hiyo katika kipindi ambacho inajiandaa na mchezo muhimu wa Kombe la FA dhidi ya Simba walikuwa na sura tofauti ya kikosi.

 

Hata hivyo, licha ya Yanga kupambana kusaka ushindi sawa na Dodoma Jiji ambao ni wenyeji ngoma ilikuwa nzito kwa timu zote ambapo zimegawana pointi moja moja.

 

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kukamilisha msimu wa 2020/21 ikiwa nafasi ya pili na pointi zake 74.

 

Dodoma Jiji inakamilisha mzunguko ikiwa nafasi ya 8 na pointi zake ni 44.

 

Kwingineko, Simba imeshinda bao 4-0 dhidi ya Namungo, Ruvu Shooting 0-1 Azam, Mbeya City 4-0 Biashara United, KMC 1-0 Ihefu, JKT Tanzania 2-1 Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons 1-1 Gwambina, Coastal Union 3-1 Kagera Sugar na Polisi Tanzania 1-0 Mwadui.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares