Yanga yailaza AFC Leopards katika mchezo wa kirafiki

271

Yanga SC imeibuka na ushindi wa goli 1-0 kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa leo Jumapili uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha dhidi ya AFC Leopards ya Kenya.

Goli la Yanga limewekwa kimiani dakika ya 83 na nahodha wa kikosi hicho, Papy Tshishimbi akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Mnyarwanda Patrick Sibomana.

Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa kutokana na uzito wa hizo timu ulishuhudia kadi nyekundu kwa mchezaji wa AFC Leopards, Vincent Obvu baada ya kuonyeshwa kandi mbili za njano kwenye mchezo wa leo.

Huu ni mchezo wa pili kwa Yanga na wa mwisho nyanda za juu kusini baada ya mchezo wa kwanza kucheza na Polisi Tanzania na ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0.

Baada ya mchezo huo, Yanga itaondoka nchini Tanzania kuelekea Gaborone Botswana kuikabili Township Rollers.

Author: Bruce Amani