Yanga yailipua Lipuli

Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya kandanda Tanzania Young Africans, imeendelea kujizolea pointi katika dimba la Taifa baada ya usiku huu wa Jumanne Oktoba 30 kupata ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Lipuli FC ya Iringa wanapaluhengo

Mshambuliaji Heritier Makambo raia wa DR Congo ndiye aliyeilipua Lipuli kwa goli safi la kipindi cha kwanza akimalizia Kazi nzuri ya mkongwe Mrisho Ngasa

Kwa ushindi huo Yanga sasa inarejea katika nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 25 ikizidiwa pointi mbili na vinara wa ligi Azam FC

Huu ni ushindi wa nane Yanga wanaupata katika uwanja wa Taifa Kati ya michezo tisa walioshuka dimbani hapo katika msimu huu wa ligi

Author: Bruce Amani

Facebook Comments