Yanga yaivamia Mbeya Ligi Kuu ya VPL, mchezo utapigwa dimba la Sokoine

237

Baada ya kutua salama Jijini Mbeya, klabu ya Yanga imekuwa sawa na kuivamia klabu mwenyeji Mbeya City kwani habari kubwa ni Yanga na mchezo wa kesho Jumamosi Februari 13 dimba la Kumbukumbu ya Sokoine.

Sasa kuelekea mtanange huo kocha mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema anaamini kesho atapata pointi tatu muhimu mbele ya wapinzani wao Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Sokoine.

Yanga ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwana nafasi ya kwanza na wana pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18.

Mbeya City haijawa na mwendo mzuri kwa msimu wa 2020/21 ambapo imecheza jumla ya mechi 18 imekusanya jumla ya pointi 14.

“Tuna wachezaji wazuri ambao wapo ndani ya kikosi imani yetu ule ushindani ambao upo nasi tutapambana kuendelea kusaka ushindi ndani ya uwanja hakuna tunachohofia.

“Kila mmoja anajua tunahitaji pointi tatu nao pia tunajua kwamba wanahitaji pointi tatu hivyo ni suala la muda kusubiri itakuaje, mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Hata hivyo, Yanga itakuwa bila kiungo mshambuliaji wao Saido Ntibazonkiza ambaye ameachwa Dar es Salaam akiendelea kuoatiwa tiba na jopo la madaktari.

Author: Bruce Amani