Yanga yajipanga kukabiliana na Wajeshi Ruvu Shooting

260

Yanga SC imesema kwenye mechi tano za Ligi Kuu nchini Tanzania ambazo itacheza ndani ya mwezi huu Disemba itahakikisha inavuna alama zote 15, wakati kimbembe hicho cha kuhesabu alama kumi na tano kitaanza mbele ya wanajeshi Ruvu Shooting Jumapili.

Timu hiyo ya Wananchi imecheza mechi 13 na kukamata usukani wa VPL kwa kufikisha alama 31 wakifutiwa na Azam FC nafasi ya pili na Simba nafasi ya tatu lakini wamepanga kuongeza wigo mpana zaidi wa pointi kwa kushinda mechi tano za mwezi Disemba.
Kuelekea mtanange wa Jumapili, Kocha wa Yanga huenda akapata nguvu mpya baada ya nahodha wake Lamine Moro raia wa Ghana kurejea mazoezini, sambamba na beki wa kulia Shomari Kibwana kufuatia kufanya mazoezi ya pamoja.
Wakati kwa Shooting chini ya mchezaji, kocha na katibu wa zamani wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa kikiwa kwenye mwendelezo mzuri wa kiwango ambapo sasa kimefikisha mechi nane za VPL bila kupoteza mechi hata moja.
Mtanange wa Jumapili utapigwa dimba la Benjamin Mkapa Novemba 6 kuanzia saa 1 kamili usiku ambapo viingilio vyake ni 5000 kwa mzunguko, 10000 VIP B&C, 15000 A 50000 Royal.

Author: Asifiwe Mbembela