Yanga yalazwa hoi na Zanaco, Wiki ya Mwananchi

Yanga imepoteza mchezo wa kirafiki kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Zanaco ya Zambia, mchezo ambao ulikuwa unahitimisha kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa baada ya utambulisho wa wachezaji mbele ya mashabiki 60,000 waliojitokeza dimba la Mkapa.

Alianza Heritier Makambo kupachika bao dakika ya 30 akimalizia pasi ya Feisal Salum Fei Toto kabla ya kusawazishwa kipindi cha pili na Hakim Mniba na lile la pili lilifungwa na Kelvin Kapumbu dk 77.

Kelvin Kaindu, Kocha Mkuu wa Zanaco amesema kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao.

Kilele cha Wiki ya Mwananchi kulikuwa na matukio mengi ikiwa ni pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kama Nandy, Mopao, Juma Nature na Temba ambao walitoa burudani za kutosha.

Pengine kupoteza mechi hiyo kunafanya iwe alamu ya kujipanga vyema kuelekea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Ligi Kuu TPL

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares