Yanga yamtimua kocha Eymael kwa kutumia lugha ya kibaguzi dhidi ya mashabiki

416

Klabu ya Yanga imemtimua Kocha mkuu wa Luc Eymael kufuatia kauli yake aliyotoa mwishoni mwa wiki ambayo ni ya kibaguzi. Eymael alinukuliwa akisema mashabiki wa Yanga ni wajinga huku akiongeza kuwa viongozi wa klabu hiyo ni waswahili walioshindwa kumtimizia matakwa yake ya kimkataba.

Kocha huyo amesema amechoka kukaa Tanzania na hana hata kifurushi cha DSTV wala gari na kuwa Yanga walimpangishia nyumba mbaya. Amedai bora tu wamwache aondoke sake na kwa mwendo huu Eymael amesema Yanga kushinda chochote.

Pia ameshangazwa na Mashabiki wa Yanga ya kutoelewa mambo ya mpira na amesema hawezi kuendelea na hayo matatizo na kufanya kazi Yanga. Mashabiki walikuwa wanamzomea na sasa anasema wao ni mambumbumbu wakupiga kelele tu na kama tumbili na kubweka kama mbwa.

Author: John Major Ouma