Yanga yatinga robo fainali Kombe la FA

Baada ya michezo minne ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuisha kwa sare na suluhu hatimaye nguvu ya Yanga imezaliwa upya katika marathon ya Kombe la Shirikisho la TFF kufuatia ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Gwambina FC katika mchezo uliopigwa leo Jumatano dimba la Uhuru.

Ushindi huo unavunja rekodi ya kutoshinda huku ikiiwezesha Yanga kufuzu hatua ya robo fainali ya FA ambapo sasa itasubili ratiba mpya kujua mpinzani wake hatua hiyo.

Bao pekee la ushindi kwa Yanga lilifungwa na kiungo mshambuliaji Haruna Niyonzima dakika ya 45 kwa shuti kali la mguu wa kushoto alilofunga akiwa nje ya18. Gwambina FC ilipambana kipindi cha pili kurudisha bao hilo uimara wa mlinda mlango Metacha Mnata na umakini wa beki kisiki Lamine Moro ulitibua mipango yao.

MCHEZO MINGINE

Azam FC imeibuka mshindi dhidi ya Ihefu kwa penati 5-4 katika mchezo uliopigwa dimba la Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

FT: Kagera Sugar 1-1 KMC (Pen: 2-0).

FT: JKT TZ 1-1 Alliance FC (Pen: 3-5)

Timu zilizotinga robo fainali ni Yanga, Azam, Kagera Sugar, Alliance, Simba, Namungo, Ndanda na Sahare

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends