Yanga yawasili Kigoma tayari kuwavaa Simba fainali ya Kombe la FA

Kuelekea mtanange wa Kombe la Shirikisho la TFF, klabu ya Yanga Leo Julai 22, 2021 imewasili Kigoma kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, itakuwa ni Jumapili Julai 25, kuanzia majira ya saa tisa alasiri.
Klabu ya Yanga inakutana na mtani wao wa jadi Simba ambao ni mabingwa watetezi wa taji hilo ambalo walitwaa msimu uliopita mbele ya Namungo.
Unatarajiwa kuwa mchezo mgumu kwa pande zote mbili kwa sababu wanakutana wakiwa wametoka kunyooshana kwenye ligi.
Julai 3, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga hivyo Yanga watataka kuendelea pale walipoishia kwenye ligi na Simba wakihitaji kulipa kisasi.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares