Yanga yaweka wazi kuachana na Lamine Moro

Yanga imeachana rasmi na aliyekuwa nahodha wake Lamine Moro Leo Alhamis Julai 29, 2021 baada ya mazungumzo ya pande mbili, Yanga na Lamine Moro.

Kuachwa kwa Lamine Moro kunaelezwa kuwa utovu wa nidhamu huenda ukawa umechangia hasa kushindwa kuelewana na kocha mkuu Nassredine Nabi wakiwa mazoezini huku jina ya mlinzi wa DC Motema Pembe, Hennock Inonga Baka likitajwa kurithi mikoba yake.
Yanga inaimarisha safu yao ya ulinzi, ambayo msimu ulioisha iliruhusu mabao 21 katika mechi 34. Ukuta wa Yanga msimu ulioisha uliundwa na Lamine Moro, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha na Adeyun Salehe.
Yanga wamethibitisha kupitia taarifa yao kamili kuwa Yanga ni wamefikia uamuzi wa kuachana na Moro ambaye ameitumikia Yanga kwa mwaka mmoja na nusu huku akiwa mkali wa mabao ya vichwa.
Msimu huu uliomalizika Moro alianza vyema kuiongoza Yanga kushinda mechi nyingi, huku akifanikiwa kuifungia timu yake mabao manne akiwa ndiye beki mwenye mabao mengi.
Inaelezwa katika makubaliano hayo Yanga na Moro wamekubaliana watalipana mshahara wa mwezi mmoja

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares