Yerry Mina kukosa mechi za awali za EPL kutokana na majeruhi

Mlinzi wa Everton Yerry Mina atakosa mechi za awali za kurudi kwa ligi kuu ya England baada ya kupata majeruhi ya misuli wiki iliyopita.

Beki huyo raia wa Colombia alitoa machozi kutokana na taarifa hiyo ya kuachwa kwenye mazoezi kwa sababu ya majeruhi.

Majeruhi hayo yanaweza kupelekea kukosa mtanange wa kwanza kabisa wa watani wa jadi dhidi ya Liverpool, ilisema taarifa kutoka ndani ya klabu.

Mina, 25, hivi sasa anaendelea kupata matibabu ya madaktari wa timu, amecheza mechi 25 tangu msimu huu kuanza, hata hivyo ripoti ya madaktari inaonyesha anaendelea vyema.

Majeruhi hayo yanakuja kipindi ambacho daktari wa Newcastle United Paul Catterson ameshatoa tahadhari juu ya uwezekano wa kupatikana kwa majeruhi kwa wachezaji kwa sababu wachezaji wanalazimika kufanya mazoezi katika vifaa maalumu vya mazoezi.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends