Yupo wapi Salah kwenye mitandao ya kijamii?

231

Mashabiki wameshangazwa leo baada ya nyota wa Liverpool Mohamed Salah kuripotiwa kufuta akaunti zake zote za mitandao ya kijamii ambako ana mamilioni ya wafuasi. Akaunti za Facebookk, Instagram na Twitter za Salah ambaye anapendwa sana nyumbani Misri na klabu yake ya Liverpool, ilifutwa bila taarifa yoyote ya kabla siku moja baada ya yeye kuweka ujumbe kwenye Twitter wenye maana fiche.

“Azimio la 2019: Wakati wa kuwasiliana, moja kwa moja,” ilisema tweet ya mwisho, ambayo picha yake ilisambazwa kote kwenye mitandao ya kijamii.

Haijafahamika wazi maramoja kama kuondolewa kwa akaunti hizo kulikuwa kwa makusudi au la. Kama ni azimio lake la mwaka wa 2019 au la, tutasubiri kuona yatakayijiri. Kinachofahamika ni kuwa Salah yuko sawa na kwa sasa analenga kuisaidia Liverpool kunyakua taji la Premier League msimu huu. Mapema mwezi huu, Salah alitajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka Afrika kwa mwaka wa pili mfululizo.

Author: Bruce Amani