Zaha aipeleka Ivory Coast robo fainali

Mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha amelipeleka taifa lake la Ivory Coast robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika baada ya kufunga goli katika mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Mali mtanange uliofanyika dimba la Suez nchini Misri.
Goli la Zaha limepatikana kunako dakika ya 76 ya mchezo baada ya piga nikupigia kwa dakika zote huku Marega na Adam Traore wa Mali wakijaribu mara kadhaa kisha kushindikana.
Ushindi wa Ivory Coast unaifanya timu hiyo kufuzu kisha itakutana na Algeria hatua ya robo fainali katika mwendelezo wa mashindano hayo. Mchezo unaofuata ni Ghana dhidi ya Tunisia Julai 8.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments