Zidane awapiku Klopp, Guardiola katika orodha ya L’Equipe ya makocha bora wa vilabu duniani

33

Zinedine Zidane ndiye meneja bora wa klabu duniani lakini bingwa wa zamani, Jose Mourinho ‘amepoteza uchawi wake’. Hiyo ni kwa mujibu wa gazeti linaloongoza la Ufaransa L’Equipe ambalo limeorodhesha makocha bora wa vilabu vya soka duniani.

Jurgen Klopp na Pep Guardiola wamewekwa na bosi wa Real Madrid Zidane katika nafasi tatu za juu huku Mfaransa Zizou akiwashinda mameneja hao wa Liverpool na Manchester City katika safu hiyo. Zidane aliongoza Real kushinda taji la LaLiga mapema mwezi huu, akishinda Barcelona ambao walikuwa wameshikilia nafasi ya kwanza kwa alama mbili kabla ya msimu kuanza tena Juni.

Mchezaji huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 49 atashuka dimbani Etihad kuumana na Guardiola mnamo Agosti 7 kwa mechi ya mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Ulaya raundi ya 16. Na licha ya kupoteza mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Guardiola huko Bernabeu mnamo Februari, L’Equipe inaamini Zidane yupo juu zaidi kuliko mkufunzi huyo wa zamani wa Barcelona.

Waliandika: Zidane ni kocha ambaye amepata kilabu moja tu, na mara chache akashindwa. ‘Kocha ambaye alifanya kile ambacho hakuna hata mmoja kati ya watangulizi wake aliwahi kufanya, alishinda Ligi ya Mabingwa mara tatu mfululizo (2016, 2017, 2018), na akarudi tena mwenyewe kuwapa ubingwa wa ligi ya Uhispania Real Madrid mwezi uliopita. ‘Guardiola ana kitu kingine, mafundisho yake, utafiti wake wa kudumu, uzuri wa uchezaji wake wa pamoja, filosofia yake (alama 198 katika misimu miwili kutoka 2017 hadi 2019), lakini hana chochote  na anachagua beki wake wa kati kama washambuliaji wake au mshambuliaji wake kama beki wa kati. ‘

Gazeti hilo lilielezea mafanikio ya Klopp ya kuwa na ‘ukakamavu‘ katika kuipa Liverpool taji lake la kwanza la ligi katika miaka 30, likimtaja kuwa ‘mtu wa mtindo’ na ‘anayependwa na wengi. Lakini pia walisema kuwa Mjerumani huyo ameshinda moja tu kati ya fainali zake tatu za Ligi ya Mabingwa, ukilinganisha na tatu za Zidane mfululizo. Mfaransa huyo alimpiga Klopp katika fainali ya 2018 kabla ya Wekundu hao kushinda Kombe hilo 2019.

Kulikuwa na sifa kidogo kwa Mourinho, aliyefafanuliwa kama “mtu aliyepitwa na wakati na aliyeisha nguvu kutokana na mapambano dhidi ya Klopp na Guardiola. Kuhusu bosi huyo Mreno, L’Equipe aliandika: ‘Hapa yuko Tottenham, anajidai mwenyewe, bado ni mzuri kwenye mazungumzo, bado yuko vizuri katika mikutano ya waandishi wa habari, bado hana mchezo wa kuvutia lakini anaonekana kuwa mbali zaidi kama maili milioni moja kutoka kwa utukufu wake wa zamani. ‘

Author: John Major Ouma