Zidane sasa asema anamtegemea Bale katika Real Madrid

Waswahili husema “Wagombanapo ndugu, wewe shika jembe ukalime” kauli hiyo ya Waswahili inasadifu vyema katika ndoa ya kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane na Gareth Bale baada ya kukubaliana kufanya kazi pamoja.

Bale alitegemewa kujiunga na Jiangsu Suning ya China mwezi Julai mwaka huu. Kuumia kwa  Eden Hazard kunafanya ndoa ya hao wawili kuzaliwa upya, jambo linaloamsha hisia kwamba huenda kesho Jumamosi anaweza akawa kwenye kikosi cha kwanza dhidi ya Celta Vigo.

“Nilitegemea angeondoka, lakini kwa sababu ameamua kubaki, nitaendelea kumuhesabu kama mchezaji wangu kama ninavyofanya kwa wachezaji wengine.”

“Bado ana mkataba hapa, ni mchezaji muhimu kwetu nadhani atatusaidia sana msimu huu”.

Hazard atakaa nje kwa wiki tatu akiuguza majeraha aliyoyapata kwenye mazoezi leo Ijumaa, Marco Asensio na mlinzi Ferland Mendy watakuwa nje mpaka mwanzoni mwa mwaka 2020 unafanya wachezaji waliokuwa wanaonekana hawafai, kuthamini.

James Rodriguez ni miongoni mwa wachezaji hao na huenda akajumuishwa kwenye kikosi cha Madrid baada ya kudumu Bayern Munich miaka miwili kwa mkopo.

Bale, 30, alicheza mechi 42 msimu uliopita licha ya kuzomewa na mashabiki timu ikicheza nyumbani, kuna uwezekano hali hiyo ikapungua au kuacha msimu huu kutokana na kukosa machaguo mengi.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends