Zlatan Ibrahimovic arejea kwenye timu ya taifa ya Sweden baada ya kutangaza kutundika daluga

Kinara wa upachikaji mabao katika Timu ya Taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic amerejea kwenye majukumu ya timu ya taifa hilo miaka mitano baada ya kutangaza kuachana na soka la kimataifa (kustaafu).

Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 39, alishafunga goli 62 katika mechi 116 za taifa lake, na alitangaza kustaafu baada ya timu yake kuondolewa kwenye hatua ya makundi ya Euro 2016.

Alifungua milango ya kurejea mwaka 2020 mwezi Novemba kupitia mahojiano na wanahabari, baada ya hapo kocha wa Sweden Janne Andersson alisafiri hadi Milan na kukutana na mshambuliaji huyo.

Ibrahimovic ana goli 14 katika mechi 14 za Serie A ndani ya uzi wa AC Milan msimu huu.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares