Zouma ajiunga na West Ham United

Wagonga Nyundo wa London, West Ham wamekamilisha uhamisho wa kumsajili beki wa kati wa Ufaransa na mchezaji wa Chelsea Kurt Zouma kwa kiasi fedha cha pauni milioni 29.8

Zouma, 26, alishinda taji la Ligi Kuu England mara mbili, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Ligi katika miaka saba aliyokaa Stamford Bridge.

Amecheza mechi nane pekee ngazi ya taifa, ambapo amewai kucheza pia kwa mkopo katika klabu ya Saint-Etienne, Stoke City na Everton.

“Ninafuraha kujiunga na klabu hii, najihisi fahari”, alisema Zouma.

Zouma alijiunga na Chelsea akiwa na miaka 19, kutokea Saint-Etienne mwaka 2014 amecheza jumla ya mechi 151 na kufunga goli 10 kwenye mashindano yote.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares