Arsenal yafikia makubaliano ya kumsaini winga wa Lille

Arsenal wamefikia makubaliano na klabu ya Ufaransa ya Lille kumsaini winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe kwa kitita cha pauni milioni 72.

Arsenal italipa kitita hicho kwa awamu kadhaa kulingana na bajeti yao msimu mpya. Makubaliano kati ya Arsenal na wawakilishi wa Pepe yanasubiri kukamilishwa.

Lakini uhamisho huo unatarajiwa kukamilishwa katika kipindi cha saa 24 na 48. Klabu ya Itali, Napoli pia ilikutana na Lille kuhusu bei ya mchezaji huyo lakini pendekezo lao likafutiliwa mbali na wawakilishi wa mchezaji huyo. Aliifungia Lille magoli 23 msimu uliopita

Author: Bruce Amani