Kocha wa Muda Tottenham Stellini Afutwa Kazi

Aliyepewa nafasi ya kuifundisha Tottenham Hotspur Cristian Stellini amefutwa kazi ya ukocha wa muda ndani ya Tottenham baada ya muda mfupi akiinoa timu hiyo mechi nne pekee.

Maamuzi ya kumfuta kazi ni baada ya timu hiyo kufungwa bao 6-1 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa uwanja wa St James Park Jumapili.

Baada ya kichapo hicho Mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy alisema haikubaliki.

Stellini, 48, alichukua timu hiyo Machi 26 baada ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Antonio Conte kukamilisha miezi 16 ya kuinoa timu hiyo.

Ryan Mason, Ndiye kocha wa muda tena wa Spurs, itakumbukwa kocha huyo alichukua mikoba ya Jose Mourinho alipofutwa kazi mwaka 2021.

Kwa sasa Spurs inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa EPL nyuma ya Newcastle United na Manchester United kwenye alama ya tatu na ya nne.

Author: Bruce Amani