Bado Naumia Kufukuzwa Kazi Chelsea – Kocha wa Bayern Tuchel

Kocha wa Bayern Munich Thomas Tuchel ameeleza kuwa kitendo cha kufukuzwa kazi katika kikosi cha Chelsea mwezi Septemba bado kina muumiza kichwa.

Kocha huyo raia wa Ujerumani amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wake wa kwanza wa Jumamosi dhidi ya wapinzani wa karibu Borussia Dortmund.

Tuchel, 49, alisema alishtushwa kupokea taarifa za kufutwa kazi.

“Ilinishtua. Niliona ni kitu cha ajabu, nilipofika uwanja wa mazoezi na kupokea taarifa za kuondolewa”, aliwaambia Wanahabari.

Tuchel alifutwa kazi kufuatia kupoteza bao 1-0 mwezi Novemba dhidi ya Dinamo Zagreb mchezo wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Wakati huo tulikuwa tumepanga na wachezaji namna ya kujikwamua ili tufanye vizuri zaidi”.

“Bado naumia nikikumbuka nilivyoondolewa. Hatupo tena karibu na watu hao (Chelsea) lakini nilishangazwa. Naipenda hii kazi, ndiyo maana naumia”.

Miongoni mwa mafanikio ya Tuchel Chelsea ilikuwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya Manchester City 2021.

Author: Bruce Amani