Bayern Yafungwa, Dortmund Yapeta Kileleni

Bayern Munich imekutana na kichapo cha bao 3-1 ugenini kwa Mainz katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga kikiwa ni kipigo cha nne msimu huu kwa mabingwa hao watetezi..

Mabao ya Mainz yamefungwa ndani ya dakika 14 tu kupitia kwa Ludovic Ajorque, Leandro Barreiro na Aaron Caricol yakiendelea kuchoma mwiba mkali kwenye viatu vya kocha mpya Thomas Tuchel ambaye ameondolewa kwenye Uefa na Kombe la Ujerumani.

Bayern walianza vyema kufunga bao la mapema ambalo lilifungwa na Sadio Mane akimalizia krosi ya Joao Cancelo kabla ya mambo kubadilika kiasi cha kuweka ubingwa wa Bundesliga kileleni hasa kwa ushindi mkubwa wa Borussia Dortmund.

Dortmund imeshinda bao 4-0 dhidi ya Eintracht Frankfurt, mabao ya Jude Bellingham, Mallen ambaye aliingia kambani mara mbili na mlinzi Mats Hummels.

Ushindi huo unaifanya BVB kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya mabingwa watetezi Bayern Munich.

Author: Bruce Amani