Dortmund, Bayern zapeta Bundesliga

Kinda wa England Jadon Sancho ameipa timu yake alama tatu katika mchezo wa Bundesliga baada ya kufunga goli pekee katika ushindi dhidi ya Freiburg.

Sancho,19, anafunga goli la saba mfululizo kwenye michezo ambayo timu yake imecheza dimba la nyumbani.

Mshambuliaji wa Arsenal kwa sasa Pierre-Emerick Aubameyang ndiye mchezaji pekee mwenye rekodi ya kufunga goli 11 mfululizo akiwa na vijana hao wa Dortmund.

Matokeo hayo yanaifanya Dortmund kuendelea kusalia nafasi ya tatu alama nne chini ya vinara Bayern Munich.

Staa Erling Braut Haaland aliingia dakika ya 63 na kushindwa kufunga goli na kuwa mara ya kwanza tangu mwezi Septemba 2018 ambapo akiwa na klabu ya Molde alishindwa kufunga dhidi ya Rosenberg.

Mbali na mchezo huo Bayern Munich imeibuka mshindi wa goli sita kwa bila dhidi ya Hoffehenm.

Ausburg 2-3 Borussia Monchengladbach

Maiz 2-0 Pardeeborn.

Author: Bruce Amani