Bayern yawekewa breki na Leverkusen

Mfululizo wake wa matokeo mazuri umefikia kikomo. Baada ya kushinda mechi nne mfululizo katika mashindano yote, Kocha Hansi Flick amepoteza mechi yake ya kwanza katika Bundesliga akiwa na Bayern Munich. Maangamizi ya Leverkusen yalifanywa na Mjamaica chipukizi Leon Bailey.

Bayern ilifungwa mabao 2 – 1 na Bayer Leverkusen mbele ya mashabiki wake wa nyumbani licha ya kuwa na nafasi chungu nzima za kufunga mabao.

Katika matokeo ya mechi nyingine za Jumamosi, Cologne ilitoka sare ya 1 – 1 na Augsburg, Borussia Dortmund wakawafunga Hertha Berlin 2 – 1, Leipzig ikakamata usukani wa ligi kwa ushindi wa 3 – 1 dhidi ya Paderborn na Hoffenheim ikatoka sare ya 1 – 1 na Düsseldorf.

Author: Bruce Amani