Bayern yamfungia Mane mechi moja kwa kukwaruzana na Sane

Nahodha wa timu ya taifa ya Senegal Sadio Mane amefungiwa kuichezea klabu yake ya Bayern Munich kwa mechi moja. Hii ni baada ya mtafaruku uliozuka kati yake na mchezaji mwenzake Leroy Sane baada ya Bayern kufungwa na Manchester City 3-0 katika mechi ya robo fainali ya vilabu bingwa Ulaya hapo juzi mjini Manchester.

Na sasa katika taarifa Bayern imesema Mane mwenye umri wa miaka 31, hatokuwepo kwenye kikosi cha Bayern katika mechi yao ya nyumbani Jumamosi, dhidi ya Hoffenheim katika Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga.

Bayern imesema sababu ya kutojumuishwa kwake ni utovu wa nidhamu kufuatia mechi dhidi ya katikati ya wiki dhidi ya Manchester City. Gazeti la Ujerumani la Bild, liliripoti kuwa Sane, alipigwa ngumi ya usoni na Mane jambo lililompelekea kukatika mdomo.

Author: Bruce Amani