Aubame kocha mpya wa Gabon

Nahodha wawili wa zamani wa timu ya taifa ya kandanda ya Gabon Pierre Aubame na Daniel Cousin wameteuliwea kuwa makocha wa timu ya Gabon, baada ya kufukuzwa Mhispania Jose Antonio Camacho wiki iliopita. Hayo ni kwa mujibu wa Shirikisho la kandanda la nchi hiyo. Aubame ni baba wa mshambuliaji wa kilabu ya Arsenal ya Uingereza Pierre-Emerick Aubameyang na Cousin liwahi kuwa mshambuliaji wa Rangers na Hull City. Camacho aliyewahi kuwa mwalimu wa timu ya taifa ya Uhispania alifukuzwa kazi baada ya Gabon kushinda michuano miwili tu kati ya 17 wakati akiiongoza kwa zaidi ya miaka miwili iliopita.

Author: Bruce Amani