Chelsea na Liverpool zatuma ujumbe

Liverpool na Chelsea ziligawana pointi tatu baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja katika uwanja wa Stamford Bridge. Daniel Sturridge, mchezaji wa zamani wa Chelsea alifunga bao safi katika dakika za mwisho mwisho na kufuta bao alilofunga Eden Hazard.

Timu zote mbili hazijapoteza mchuano mpaka sasa katika ligi ambapo Liverpool wako nyuma ya mabingwa Manchester City kwa tofauti ya mabao na Chelsea katika nafasi ya tatu na pengo la pointi mbili.

Haya hapa mambo matatu yaliyojitokeza kwenye mechi hiyo ya kusisimua.

Sturridge alifunga bao safi la kusawazisha

Mohamed Salah alichaguliwa na FIFA mbele ya Eden Hazard kama mchezaji wa tatu bora duniani mwaka jana kndo na kushinda tuzo za mchezaji bora wa mwaka msimu uliopita.

Lakini hakuna shaka kuhusu nani ambaye kwa sasa ni mchezaji bora kwenye ligi baada ya Hazard kufunga bao lake la saba la msimu, wakati Salah alishindwa kutumia nafasi tatu za wazi katika mechi ya jana.

Kocha wa Chelsea Sarri anampa changamoto Hazard kuyafikia mafanikio ya Salah ya msimu uliopita na kufunga mabao 40 kwa mara ya kwanza katika taaluma yake

Mpambano huo uliwaleta pamoja makipa wawili wenye gharama kubwa kabisa duniani. Kepa Arrrizabalaga na Alisson Becker walionyesha jana ni kwa nini mamilioni yalitumiwa kuwekeza katika huduma zao.

Sarri alisisitiza msimu mzima kuwa tmu yake itakuwa nyuma ya City na Liverpool ambazo ziko katika misimu yao ya tatu chini ya Pep Guardiola na Klopp wakati Chelsea ikijizoesha na mfumo wa Muitaliano huyo.

Hata hivyo, hata kocha huyo wa Napoli amekiri kuwa Chelsea “wako karibu” kuliko alivyotarajia baada ya kukutana na Liverpool mara mbili katika siku nne na kukaribia kupata ushindi mara mbili.

Wakati Hazard na viungo Jorginho, Kante na Kovacic wameshamiri katika wiki za mwanzo za msimu, kuna wasiwasi katika ulinzi. Hata hivyo David Luiz na Antonio Rudiger walifanya kazi safi katika kuizuia Liverpool.

Author: Bruce Amani

ChelseaHazardKloppLiverpoolSalahSarri