Kerr achukua mikoba ya Black Leopards ya Afrika Kusini

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Gor Mahia nchini Kenya Dylan Kerr ameajiriwa na klabu ya Afrika Kusini Black Leopards.

Raia huyo wa Uingereza, aliyejizulu kutoka Gor Mahia, anachukua nafasi ya Joel Masutha aliyeachia nafasi hiyo wili iliyopita kwa sababu ya matokeo mabaya.

Kerr anachukua uongozi wa klabu ambayo inashikilia nafasi ya 14 kati ya klabu 16 zinazoshiriki ligi kuu ya soka nchini Afrika Kusini, na kazi kubwa ni kuisaidia kupanda hadi katika nafasi za juu, katika msururu wa ligi kuu.

Author: Bruce Amani