Man United yanusurika kipigo cha Southampton

Manchester United imeshindwa kuendelea na mwanzo bora wa Ligi Kuu England baada ya leo kubanwa mbavu na Southampton ukiwa ni mchezo wa pili baada ya ule wa Leeds United. Imelazika kutoa sare ya 1-1.

Kocha Ole Gunnar Solskjaer baada ya kuonekana kukiimarisha kikosi kwenye mechi iliyopita kabla ya leo baada ya ushindi wa goli 5-1 dhidi ya Leeds, mbele ya Southampton walikuwa hoi kiasi kwamba wangepoteza mtanange huo.

Bao la Southampton lilipatikana kufuatia kiungo mkabaji Fred raia wa Brazil kugusa shuti la Che Adams na kumshinda mlinda mlango David de Gea ambaye anaruhusu bao lake la pili.

United walisawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji kijana Mason Greenwood ambaye mpira wake ulimshinda mlinda mlango Alex McCarthy.

Ni matokeo mabaya kwa kocha Ole Gunnar Solskjaer, lakini ni matokeo mazuri kwa Southampton ambao walitoka kufungwa na Everton mtanange wa ufunguzi wa Ligi.

Author: Bruce Amani