Manchester City kuwakosa Jesus, Aguero kutokana na majeruhi

Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa takribani wiki tatu akiuguza majeruhi aliyoyapata akikitumikia kikosi cha City.

Staa huyo wa Brazil alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ambayo itaingia kambini kujiwinda na  mechi mbili dhidi ya Bolivia na Peru lakini ameshatolewa.

Shirikisho la Soka nchini Brazil limethibitisha kumkosa strika huyo katika mechi hizo mbili.

Jesus, 23, alipata majeruhi kwenye mchezo wa Jumatatu dhidi ya Wolves ambapo alicheza dakika zote 90 na alifunga goli pia katika mtanange huo.

Wakati huo huo, strika mweza Manchester City Sergio Aguero anatarajia kukosa wiki nyingine saba akiwa na majeruhi ya goti.

Man City watakutana na Leicester City siku ya Jumapili majira ya saa 12 :30 jioni.

Author: Asifiwe Mbembela