Mshambuliaji wa Serengeti boys aelekea Afrika Kusini

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ya chini ya miaka 17 (Serengeti Boys), Kelvin John ameanza safari jioni ya leo Jumatatu kuelekea Afrika Kusini katika klabu ya Ajax kufanya majaribio ya wiki mbili

Kelvin alirejea nchini akitokea Denmark alikokua katika majaribio katika klabu ya vijana ya HB Koge inayoshiriki ligi daraja la kwanza, akiwa anasubiria majibu yake ameamua kwenda kutafuta fursa kwingineko.

Kelvin amekuwa mchezaji wa pili kutoka kikosi cha Serengeti Boys baada ya hapo awali kinda na nahodha wa kikosi hicho Morice Abraham ambaye naye alienda kwenye majaribio katika klabu ya Midtyland.

Kelvin, mwenye umri wa miaka16, alikuwa Denmark kwa zaidi ya wiki tatu akifanya majaribio katika timu hiyo ambapo alirejea Tanzania kabla ya kuondoka kuelekea huko Bondeni kwa Madiba.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kelvin John ameandika “Ndio naelekea sauzi, majaribio Ajax kupitia Ajax Cape Town”

Ajax inashika nafasi ya nane katika msimamo wa ligi kuu Afrika ya Kusini ikiwa na alama 15 katika michezo kumi na moja.

Author: Bruce Amani