Scott McTominay ajifunga mkataba wa miaka 5 Manchester United

Kiungo mkabaji wa Manchester United Scott McTominay ameongeza kandarasi mpya ya kuendelea kusalia ndani ya Mashetani Wekundu hao, na sasa mkataba wake utamalizika Juni 2025.

Dili hilo linakuja kipindi ambacho zao hilo la akademia ya Manchester United limekuwa na mwendelezo mzuri tangu apandishwe timu ya wakubwa katika mchezo dhidi Manchester United Mei 2017.

Mctominay ni mzaliwa wa Scotland katika mji wa Lancaster mwaka 1997, na amecheza mechi 75 na kufunga goli sita za EPL moja wao ni lile dhidi ya Manchester City katika ushindi wa goli 2-0 mwezi Marchi.

“Sijui kitu kingine ila Manchester United, natumai hali hii ya upambanaji kwenye klabu hii utaendelea kwa kitambo kirefu zaidi” alisema baada ya kutia saini mkataba huo mpya”.

Author: Bruce Amani