Tanzania U-23 yatinga fainali Cecafa 2020

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana wa chini ya umri wa miaka 23 imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge U23) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan Kusini, mtanange uliopigwa dimba la Bahir Ethiopia Julai 28.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Kelvin Nashon Naftali dakika ya 64 na sasa Tanzania itamenyana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili Burundi ambaye amepita hapo kwa kuifunga Kenya kwenye mikwaju ya penati.

Mechi ya Fainali itafanyika Ijumaa baada ya kutafutwa mshindi wa tatu baina ya Sudan Kusini dhidi ya Kenya siku hiyo hiyo ya Ijumaa na dimba hilo hilo Bahir.

Author: Asifiwe Mbembela