Yanga yatupwa nje, Azam yatinga nusu fainali Kombe la Mapinduzi

Mabingwa watetezi wa taji la Mapinduzi Azam FC imefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuchomoza kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya vijana wa KVZ ya Zanzibar

Azam timu ambayo inapewa nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wake msimu huu kutokana na ubora na uimara wa kikosi chake, hawakupata ushindi huo kilelemama ilibidi wapambane ilikuibuka kidedea baada ya KVZ kupata goli la utangulizi katika kipindi cha kwanza

Kipindi cha pili mshambuliaji wake hatari Donald Ndombo Ngoma aliisawazishia Azam kunako dakika ya 75 akimalizia mpira wa pasi muruwa ilipenyezwa na Zambia Obrey Chirwa

Azam waliendelea kulisakama lango la KVZ na kufanikiwa kupata goli la pili na la ushindi kupitia kwa mshambuliaji Obrey Chirwa

Kwa ushindi huo Azam imefikisha pointi saba wakiwa kileleni baada ya kushuka dimbani Mara 3 na wamesalia na mchezo mmoja

Wakati Azam wanatinga nusu fainali vinara wa ligi kuu ya bara Young Africans wameondoshwa katika michuano hiyo na timu ya Malindi baada ya kulala kwa mabao 2-1 katika mchezo uliokuwa na mabao ya kusisimua

Licha ya kuanza kuandikisha bao la kwanza Yanga hawakuweza kufua dafu kwa timu hiyo kongwe toka Zanzibar Malindi kwa kuruhusu goli la kusawazisha kwa mkwaju mkali na timu hizo kwenda likizo fupi ama mapumziko zikiwa sare ya goli 1-1

Kipindi cha pili Malindi iliidai chenji Yanga na kukubali kuipa goli la pili hivyo mchezo huo kumalizika magoli  malindi 2-1 Yanga.

Kwa matokeo hayo Malindi inafikisha alama saba sawa na Azam huku Yanga ikisalia na alama tatu na mchezo mmoja wa kukamilisha ratiba dhidi ya Jamhuri

Author: Bruce Amani