Yanga yaifumua Tukuyu Stars katika Kombe la Shirikisho la Azam

Klabu ya Yanga imeanza vyema mashindano ya kombe la shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuifumua klabu ya ‘Wanyambala’ kutoka Tukuyu, Tukuyu Stars kwa goli 4-0 katika mtanange  uliofanyika katika dimba taifa jijini Dar es Salaam.

Tukuyu Stars ambayo imewai kushinda taji la ligi daraja la kwanza (ligi kuu kwa sasa) mwaka 1985/86 ilionekana kuimarika zaidi kipindi cha kwanza kabla kipindi cha pili kutepeta ingawa vipindi vyote viwili ilikukubali goli mbili kwa kila kimoja.

Ushindi wa Yanga umekuja kupitia kwa Amis Tambwe aliyefunga magoli matatu huko goli moja likiwekwa kimiani na Mkongomani, Heritier Makambo ambaye hata kwenye ligi kuu Tanzania bara anafanya vizuri akiwa amefunga goli  9 katika michezo 17 iliyocheza.

Kwa upande wa Amis Tambwe anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli tatu katika mashindano ya ASFC na ni hat trick.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga iweze kuendelea kusalia kwenye mashindano kutokana na ushindi wa leo. Wakati huo Wanyambala Tukuyu Stars wameaaga rasmi mashindano kwa kupokea kisago hicho cha idadi hiyo kubwa ya mabao.

Baada ya mchezo wa leo Yanga sasa inajiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbeya city utakayofanyika tarehe 29 mwezi huu wakati Tukuyu Stars inarudi kuendelea kushiriki ligi daraja la pili.

Author: Bruce Amani