Yanga Yaingia Anga za Kupinga Mmonyoko wa Maadili

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kupitia kwa Waziri Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima imeingia kwenye makubaliano na klabu ya Yanga kwa ajili ya kupinga na kutokomeza mmomonyoko wa maadili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto.

Makubaliano hayo ya pande mbili yamefikiwa Leo Ijumaa Aprili 14, 2023 wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari kilichofanyika Ukumbi wa Wizara ambapo mategemeo ya Wizara ni kuona unyanyasaji unaoungua.

“Napenda kuchukua fursa hii kuwatambulisha rasmi Klabu ya Young Africans SC kuwa Mabalozi wa kampeni ya kupinga na kutokomeza mmomonyoko wa maadili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto”, alisema Dkt. Gwajima.

Rais wa klabu ya Yanga Hersi Ally Said akizungumzia makubaliano hayo amezisihi klabu nyingine kuonyesha ushirikiano wa kushiriki katika kampeni hiyo ya kupinga mmonyoko wa maadili.

“Napenda kutoa rai kwa vilabu vya Simba SC, Azam FC, KMC na vingine vyote kuunga mkono kampeni hii, kampeni hii siyo mashindano ya kibiashara sote kwa pamoja tuungane na Mhe. Waziri kutokomeza changamoto hizi kubwa na kuilinda jamii yetu” alisema Mhandisi Hersi.

Aidha, Rais huyo amesema kama klabu zenye wafuasi wengi watashindwa kushiriki katika kampeni kama hizo, ukatili utaendelea kwa watoto na wanawake.

Author: Asifiwe Mbembela