KMC Yamfurusha Kocha Hitimana, Julio Apata Shavu

KMC imefikia maamuzi ya kumfuta kazi Kocha Mnyarwanda, Thierry Hitimana na wasaidizi wake wote nafasi yake imechukuliwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye anaingia na wasaidizi wake kuanzia sasa.

Hitimana anaondolewa kufuatiwa mwenendo mbaya wa timu, hadi sasa ikiwa inashika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 26, ikifuatiwa na Ruvu Shooting pointi 20 na Polisi Tanzania pointi 19.

Mwishoni mwa msimu timu mbili zitakazoshika nafasi za mwisho, 15 na 16 zitashuka moja kwa moja wakati mbili za juu ya hapo zitacheza michezo miwili ya mtoano na timu kutoka daraja la kwanza.

Author: Asifiwe Mbembela