Adhabu ya Bingwa wa Olimpiki Mkenya Sumgong yarefushwa

Bingwa wa mbio ya marathon katika mashindano ya Olimpiki Mkenya Jemima Sumgong amepigwa marufuku ya miaka minane baada ya kutuhu,iwa kwa kudanganya katika kesi yake ya awali ya matumizi ya dawa zilizopigwa maruku michezoni.

Sumgong tayari alikuwa amepigwa marufuku kwa miaka minne baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kuongeza misuli nguvu mwaka aina ya EPO mwaka wa 2017, lakini sasa atafungiwa kushiriki mashindano hadi mwaka wa 2027 baada ya kiengo cha uadilifu cha IAAF kutoa uamuzi kuwa aliwasilisha makusudi maelezo ya uwongo ya kutitembelea hospitali ili kufafanua vipimo vilivyogundua matumizi ya dawa hizo zilizopigwa marufuku.

Sumgong alifikisha umri wa miaka 34 mwezi uliopita, kumaanisha kuwa itakuwa vigumu kwake kurejea tena katika mashindano baada ya adhabu hiyo kukamilika.

Sumgong, aliyebatilisha kesi nyingine ya rufaa dhidi ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli mwaka wa 2012, alikuwa Mkenya wa kwanza mwanamke kushinda mbio ya marathon katika Olimpiki wakati aliponyakua dhahabu katika Michezo ya Rio de Janeiro mwaka wa 2-16. Alishinda London marathon mwaka huo huo.

Author: Bruce Amani