Droo ya hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika kufanyika

Mbivu na mbichi za nani na wapi mabingwa wa ligi kuu ya kandanda nchini Tanzania Simba Sports Club watacheza katika michuano ya klabu bingwa Afrika kujulikana leo.

Simba ilifanikiwa kufuzu baada ya kuitoa Mbabane Swallows kwa idadi ya goli 8-0 katika mchezo wa kwanza hatua ya awali kabisa, kabla ya kuitoa Nkana FC kutoka Zambia kwa jumla ya goli 4-3 kwa raundi zote mbili.

Katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati Simba ni timu pekee ambayo imefanikiwa kuingia hatua ya makundi ya klabu bingwa baada ya timu nyingine kuondolewa kama JKU, Gor Mahia na nyinginezo.

Ratiba ya upangaji wa makundi inategemewa kuanza majira ya saa moja kamili jioni kwa masaa ya Afrika Mashariki katika mji wa Cairo Misri ambapo Simba imewakilishwa na Mwenyekiti wao Sweddy Mkwabi.

Timu ambazo zimefuzu na zinasubiri  makundi ni pamoja na TP Mazembe, Mamelody Sundown, ES De Tunis, Costantine, Ismaily, Al Ahly, As Vita Club,  Asec Mimomas, Saoura, Club Afrikan, Orlando Pirates, Al Wydad, Horoya, Fc Platinum na Lobi Stars.

Katika droo hiyo kila kundi litashrikisha timu nne, michezo mitatu uwanja wa nyumbani na mitatu uwanja wa ugenini. Mechi ya klabu bingwa zinategemewa kuanza kuchezwa kuanzia Januari 12, 13, na 14 mwaka ujao.

Author: Bruce Amani