Aguero aula mkataba wa miaka miwili Barcelona

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Kun Aguero amejiunga na atatambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa FC Barcelona wiki hii baada ya mkataba wake na Man City kukamilika Jumatatu ya Leo Mei 31.
Mchezaji huyo raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 32, anaondoka Manchester City baada ya kuitumikia kwa miaka 10 ambapo katika kipindi hicho amegeuka kuwa mfungaji bora akiwa na bao 260 mechi 390.
Mchezo wa mwisho kwa Aguero ulikuwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea ambapo walipoteza kwa bao 1-0.
Tayari mkataba mpya wa miaka miwili na Barcelona umefikiwa, ambapo Aguero amewekewa kipengele cha timu inayohitaji huduma yake kulipa kiasi cha pauni milioni 86 (Euro 100) kama sehemu ya fidia.
Aguero, anaondoka akiwa ameshinda mataji 15, anajiunga Barca na atakutana na rafiki yake Lionel Messi ambaye pia ni raia wa Argentina.

Author: Bruce Amani