Bale aipa Real ushindi dhidi ya Huesca

Mshambuliaji wa Real Madrid ambaye ni raia wa Wales Gareth Bale aliipa timu yake alama zote tatu kupitia goli alilolifunga dhidi ya Huesca katika mchezo ambao Madrid ilizidiwa kwa kiasi kikubwa.

Goli hilo lililofungwa kipindi cha kwanza limemaliza ukame wa magoli kwa Gareth Bale ambaye alikuwa amecheza michezo 10 bila kufunga hata goli moja.

Huesca iliyoonekana kuimarika zaidi katika mchezo huo ilitengeneza nafasi kadhaa za kusawazisha goli kupitia kwa Gonzalo Malero alipopiga kichwa kilichoenda nje sentimita chache kutoka mtambaa wa panya.

Goli la Bale alipiga shuti kali ambalo lilimshinda mlinda mlango. Kama si bahati basi Huesca ingeweza kushinda baada ya mashuti yote mawili ya dakika za mwisho kuzuiliwa na mlinda mlango Thibaut Courtois na mlinzi Dani Carvajal.

Ikiwa ni mara ya kwanza kwa msimu huu kucheza La Liga, Huesca ilionyesha jitihada kubwa baada ya kupata mashuti manne yaliyolenga goli na mengine kutoka nje ya goli..

Huku Real Madrid akiambulia mashuti mawili tu yaliyolenga goli katika Kipindi cha pili, yakiwa ni machache zaidi tangu msimu kuanza, mshambuliaji wa timu hiyo Karim Benzema akishindwa hata kupiga shuti moja. Matokeo hayo yanaifanya Madrid kuwa nyuma ya Barcelona na pengo la pointi tano. Barca inaongoza ligi baada ya kuikandamiza Espanyol 4-0.

Author: Bruce Amani