Yanga yapata ushindi wa jasho dhidi ya KMC

Goli la jioni la kiungo fundi Feisal SALUM Fei Toto, limeipa Yanga pointu tatu muhimu katika mchezo mgumu dhidi ya vijana wa KMC na kurejea katika nafasi ya pili ikiwa na alama 22 baada ya kushuka dimbani mara 8

Mashabiki wa Yanga ambao walizizima kwa muda mrefu uwanjani kutokana na ugumu wa vijana wa KMC ilibidi wasubiri mpaka dakika ya 89 Ndio waliamsha nderemo baada ya kupata uhakika wa kuondoka na pointi zote tatu na kuendeleza rekodi ya kukupoteza katika michezo ya ligi kuu msimu huu

Wakicheza bila ya wachezaji wao tegemeo Ibrahim Ajib na Papy Kabamba Tshitshimbi Yanga ilishindwa kuleta faraja kwa mashabiki wake mpaka pale walifunga goli katika dakika za lala Salama

Licha ya kuondoka na pointi tatu lakini mashabiki wa timu hiyo hawakuridhika na kiwango cha timu yao hivyo wametoa wito kwa benchi la ufundi kufanyia kazi mapungufu yaliyo jitokeza katika mchezo huo ili waweze kundeleza wimbi la ushindi katika ligi kuu msimu huu

Author: Bruce Amani

Yanga