Glazer wa Man United, Henry wa Liverpool wajishusha kwa mashabiki kwa kujiunga na European Super League

Mmiliki wa klabu ya Manchester United Joel Glazer na yule wa Liverpool John Henry wamewaomba msamaha mashabiki wa klabu hizo kutokana na kuweka wazi mpango kujiunga na European Super League.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida kwa wamiliki hao kutoka nje ya umma na kuzungumza, wawili hao kwa nyakati tofauti wamesema mpira wa miguu bila mashabiki haiwezekani na ni muhimu kuwepo.

United, Liverpool na vilabu vingine vinne vya England waliweka wazi Jana Jumanne kujitoa rasmi kwenye mpango wa kushiriki michuano mipya inayofahamika kwa jina la European Super League ESL.

“Hatukuonyesha heshima inayowastahiri mashabiki wetu ” alisema Glazer katika barua ya wazi iliyotolewa na klabu ya Manchester United.

Mapema Leo Jumatano, Henry alisema “tumewakosea vya kutosha mashabiki wetu, soka si chochote bila uwepo wenu (mashabiki)” alisema.

Mwenyekiti wa Juventus Andrea Agnelli alisema Ligi hiyo mpya haitaendelea baada ya klabu zote sita kujitoa kwenye michuano hiyo.

Klabu ya AC Milan, Inter Milan na Atletico Madrid wamejitoa leo kufuatia vilabu vya EPL kujiweka kando.

Henry alipeleka msamaha wake kwa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, wachezaji pamoja na viongozi wengine ndani ya Majogoo wa Jiji la Merseyside.

Author: Bruce Amani