Andreas Pereira wa Manchester United atua lazio kwa mkopo

Kiungo mshambuliaji wa Manchester United Andreas Pereira amekubali kujiunga na Lazio kwa mkopo wa msimu mzima klabuni hapo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, alijiunga na Manchester United mwaka 2014 lakini hadi sasa ameshindwa kulishawishi benchi la United.

Hata hivyo, kwa kipindi chote hicho alikuwa akikitumikia kikosi cha Granada na Valencia kwa mkopo katika nyakati tofauti.

Katika msimu wa kwanza wa Ole Gunnar Solskjaer alikuwa alionekana anaenda kuwa chaguo la kwanza ambapo alicheza mechi 40 katika msimu wa mashindano.

Author: Bruce Amani