Inter Milan yakamilisha usajili wa Alexis Sanchez wa Manchester United

Inter Milan wamekamilisha usajili wa moja kwa moja wa staa wa Manchester United na Chile Alexis Sanchez kwa kandarasi ya miaka mitatu. Nyota huyo raia wa Chile mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na klabu hiyo ya Serie A kwa mkataba wa mkopo 2019.

Amefunga goli nne katika mechi 29 za mashindano yote. “Tumekubali aondoke klabu hapa” alisema kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer siku ya Jumatano baada ya mchezo wa 16 bora dhidi ya LASK dimba la Old Trafford.

“Amekuwa na wakati bora pale. Ni mchezaji bora lakini kutokana na sababu ambazo hakuna ajuaye kwanini hatukupata ubora wake tukiwa naye. Tunamtakia kila la heri” aliongeza mchezaji huyo wa zamani wa United.

Makubaliano binafsi hayajawekwa wazi lakini United wamekubali kumuachia ili kujiimarisha kiuchumi baada ya anguko uchumi lililochagizwa na Covid-19. Ndani ya Manchester United Alexis Sanchez alicheza mechi 45 baada ya kujiunga nayo akitokea Arsenal mwaka 2018 akiwa amefunga goli 5 pekee.

Anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Inter Milan baada ya miezi 12 tu, Romelu Lukaku na Ashley Young ni miongoni mwao.

Author: Asifiwe Mbembela