Tetesi za Mastaa Ulaya: Man City Yaandaa Mkataba Mpya wa Haaland

Manchester City wanaandaa mkataba bab kubwa kwa mshambuliaji wake wa kimataifa wa Norwei Erling Braut Haaland, 22, katika kandarasi mpya itakayoondoa kipengele ambacho kilikuwa kinamruhusu mchezaji huyo kuondoka Manchester City kwa dau la pauni milioni 150.

Chelsea imeondoa uwezekano wa kumchukua kocha wa zamani wa Hispania Luis Enrique ambapo maamuzi yamebakia kwa kocha wa zamani wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino ambaye kwa sasa hana timu.

Manchester United wanavutiwa kumsajili beki wa kulia wa Bayer Leverkusen na Uholanzi Jeremie Frimpong, 22, ambapo United wanahitaji kuachana na Aaron Wan-Bissaka, 25, na beki wa Ureno Portugal’s Diogo Dalot, 24.

Rais wa La Liga Javier Tebas amesema Barcelona haitakuwa na uwezo wa kumsajili tena Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi 35, kutokana na hali ya kiuchumi ya klabu hiyo kwa sasa.

Author: Bruce Amani